MAJIBU YA MASWALI YANAYOULIZWA MARA KWA MARA NA WANAFUNZI WANAOTAKA KUJIUNGA NA CHUO CHA AFYA NA SAYANSI SHIRIKISHI CHA PADRE PIO (PCoHAS FAQ & A)
- Chuo kimesajiliwa?
Ndio, Chuo kimesajiliwa na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) kwa namba ya Usajili HAS/ 186 na kutambuliwa na Wizara ya Afya. Unaweza kutembelea Tovuti ya NACTVET kwa uthibitisho https://www.nacte.go.tz/index.php/registration/registered institutions/institute/18084602030205/.
2. Chuo kinamilikiwa na taasisi ya dini au binafsi?
Chuo cha PADRE PIO ni Chuo kinachomilikiwa na taasisi binafsi ya PADRE PIO TANZANIA COMPANY. Chuo chetu kinafuata maadili na maisha ya Mtakatifu Padre Pio ambaye historia inamkumbuka katika kusaidia watu wenye Uhitaji wa kiafya na kiroho.
3. Chuo kinapatikana wapi na kina kampasi ngapi?
Chuo kinapatikana Manispaa ya Temeke, katika Kampasi zake mbili ambazo ni Temeke iliyopo Mkabala na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke na Buza, karibu na Mnarani.
4. Chuo kinatoa kozi zipi na ni za muda gani?
Chuo kinatoa kozi tatu (3) ambazo ni Utabibu (CO), Ufamasia (PST) na Ustawi wa Jamii mpaka ngazi ya Diploma, ambapo zinachukua muda wa miaka mitatu mpaka kuhitimu ngazi ya Diploma.
5. Naomba kufahamu Sifa za kujiunga na chuo.
Sifa za kujiunga zinategemea na aina ya kozi / fani. Mfano;
S/No. | Kozi | Vigezo vya kujiunga |
1. | Utabibu (Clinical Medicine) | Ufaulu wa angalau alama D Nne, ambapo D tatu lazima ziwe za masomo ya Fizikia, Kemia na Biology |
2. | Ufamasia (Pharmacy) | Ufaulu wa angalau alama D Nne, ambapo D mbili lazima ziwe za masomo ya Kemia na Biology |
3. | Ustawi wa Jamii (Social Work) | Ufaulu wa angalau alama D Nne, katika masomo yeyote isipokuwa somo la Dini. |
6. Je nikitaka kujiunga na Chuo chenu, natakiwa kufuata utaratibu gani?
Kwa mwanafunzi anayetaka kujiunga na Chuo chetu anaweza kufuata taratibu/ njia zifuatazo;
i. Kufika katika ofisi za Chuo zilizopo Mkabala na Hospitali ya Temeke au Kampasi ya Buza. Kuwasiliana na afisa udahili kupitia Na. 0757 743547 | 0679 743 547 |0736 743 547 | 0694 834 034 ili kuweza kutumiwa fomu ya maombi kwa njia ya WhatsApp. Unaweza kutembelea Tovuti / Website ya Chuo www.pchohas.ac.tz na kupakua fomu ya Maombi ya Udahili na nyaraka nyingine. ii. Unaweza pia kufanya maombi kwa njia ya mitandao (Online Application System) kwa kutembelea Tovuti yetu www.pcohas.ac.tz
7. Ada ni kiasi gani kwa mwaka?
Jibu; Ada inategemea na kozi unayotoka Kusoma, Mfano;
S/N | Kozi | Ada (Tsh.) |
1. | Utabibu | 2,000,000 |
2. | Ufamasia | 1,900,000 |
3. | Ustawi wa Jamii | 800,000 |
8. Ada inalipwa Kwa awamu ngapi kwa mwaka?
Jibu: Ada inalipwa kwa Awamu Nne
9. Kuna michango mingine mbali ya Ada?
Ndio; Mwanafunzi anawajibika kulipia michango mingine (other charges) kama ilivyoainishwa katika Fomu ya Maombi ya Chuo (Admission Form) na Fomu ya kujiunga na Chuo (Joining instruction Form).
10. Mwanafunzi akichelewa kulipa Ada anaweza kusaidiwa?
Ndio. Wanafunzi wenye changamoto za Ada wanaweza kupewa utaratibu mzuri wa namna ya kukamilisha malipo yao, endapo taarifa zitatolewa kwa wakati.
11. Kuna gharama za mitihani ya ziada (supplementary examination)?
Ndio; Mwanafunzi anawajibika kulipia gharama za mitihani ya marudio (supplementaries), na mitihani Maalum (special examinations) kiasi cha Tsh. 50,000 kwa mitihani.
12.Chuo kina Hostel, na zinapatikana karibu na Chuo?
Ndio, Chuo kina Hostel zilizopo karibu na Mazingira ya Chuo. Hostels ni salama na zina mazingira safi.
13.Naomba kufahamu Gharama za Hostel?
Hostel zinatolewa bila malipo kwa wanafunzi wote wanaoanza mwaka wa kwanza, isipokuwa atachangia Gharama za Umeme, Maji na Usafi zitatolewa na Mwanafunzi husika kiasi cha Tsh. Elfu Kumi (10,000) kwa Mwezi.
14.Chuo kinatoa chakula?
Ndio; Chuo kina utaratibu wa kutoa huduma ya chakula kwa mwanafunzi anayehitaji ambayo ni Tsh. 5000 tu kwa siku. Jumla ya Fedha ya Chakula kwa mwaka ni Tsh. 1,500,000 ambayo inalipwa kwa awamu mbili.
15. Chuo kina huduma ya usafiri?
Ndio; Chuo kina usafiri kwa ajili ya kuwezesha wanafunzi kwenda katika vituo vya mafunzo kwa vitendo ambavyo viko mbali.
16. Chuo kina walimu wa kutosha na ufundishaji wake ni mzuri?
Chuo cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Padre Pio kina waalimu waliobobea na wenye mafunzo ya mbinu za ufundishaji (teaching methodology). Pia Waalimu wamesajiliwa na Mabaraza ya Taaluma na kutambuliwa na NACTVET na Wizara ya Afya.
17. Naomba kufahamu kuhusu Ufaulu wa Chuo?
Chuo cha PADRE PIO ni Chuo pekee katika Mkoa wa Dar-es-salaam ambazo kinaongoza kwa Ufaulu mzuri wa wanafunzi wake. Pia ni miongoni mwa Vyuo vichache vyenye sifa ya kutoa Mafunzo bora, na kutoa Wahitimu wenye ujuzi na maarifa ya kutosha.
18. Mwanafunzi anapataje sehemu za kufanya elimu kwa vitendo (field and practical training)?
Chuo kinawajibika kuhakikisha wanafunzi wote wanapata vituo vya kufanya mafunzo kwa vitendo. Pia Chuo kinahakikisha Wanafunzi wanapata usimamizi wa karibu wa wataalamu ili kujifunza vizuri.
19. Chuo kina maabara za kutosha kufanyia mafunzo kwa vitendo?
Ndio; Chuo kina Maabara tatu (3) za kujifunzia zinazoenda sambamba na idadi ya Wanafunzi. Kuna Maabara ya Ufamasia, Maabara ya Utabibu na Maabara ya Komputa.
20. Chuo kinatoa huduma ya Mtandao (internet) kwa wanafunzi?
Ndio; Chuo kinatoa huduma ya mitandao katika maeneo ya Maktaba, na maeneo maalumu kwa ajili ya kujisomea. Hii inapenda sambamba na kompyuta kwa wanafunzi kwa ajili ya kujifunzia?
21. Je, Chuo kina Utaratibu wa Mavazi (Dressing code)
Ndio; Chuo kinafuata Mwongozo wa Mavazi ya Wanafunzi katika Vyuo vya Afya Kada za Kati Tanzania Bara wa Septemba 2020. Katika kuhakikisha utekelezaji wa Mwongozo huu, Mwanafunzi anatakiwa kupata Sare kutoka Chuo na si vinginevyo.
22. Chuo kuna sehemu za kufanyia ibada?
Ndio; Chuo kinatoa fursa kwa dini, na madhehebu yote kuendesha shughuli za Ibada ndani ya Eneo la Chuo.
23. Je chuo kinapokewa wanafunzi katika muhula wa mwezi wa tatu?
Ndio; Chuo kinapokea wanafunzi katika dirisha la udahili la Mwezi wa Tatu kwa kozi ya Ustawi wa Jamii pekee. Kwa sasa NACTVET imesitisha udahili katikawa dirisha hili kwa kozi za Utabibu na Famasia. Tutawajulusha mapema iwezekanavyo endapo utaratibu wa awali utarejeshwa.
24. Chuo kinaruhusu wanafunzi kuhamia na kuhama?
Ndio; Ni haki ya kila mwanafunzi kuhamia au kuhama, baada ya kufuata kanuni na masharti yaliyowekwa na NACTVET.
25. Masomo yanaanza muda gani na yanaisha muda gani, Kuna vipindi vya jioni?
Muda wa masomo kwa mujibu wa mitaala ya Wizara ya Afya ni kuanzia Saa 2 Asubuhi na Mpaka Saa 10 Jioni. Mara chache inaweza kupelekea vipindi kuisha kwa kuchelewa na kuanza mapema.
26. Masomo yanaanza lini?
Kwa kawaida Chuo kinafuata kalenda ya Masomo ya Wizara ya Afya, ambapo mara nyingi Vyuo vyote huanza masomo katika Mwezi Oktoba wa kila mwaka.
27. Je chuo kinatoa fursa ya ushindani katika michezo?
Ndio; Chuo chetu kina viwanja vya michezo kwa ajili ya kutoa fursa ya wanafunzi kushiriki michezo mbalimbali. Kupitia Bonanza linalofanyika kila Mwaka ambapo wanafunzi wanashindana katika michezo. Pia Chuo chetu kinashiriki michezo kwa ushirika na Vyuo vingine vya Afya.
28. Je chuo kina utaratibu wa kutoa motisha kwa Wanafunzi Wanaofanya Vizuri?
Ndio; Chuo kinatoa simu aina ya tablet mpya kwa wanafunzi watatu Wanaofanya vizuri zaidi kwa kila darasa.
29. Je chuo kinamsaidia vipi mwanafunzi kupata ajira?
Ndio; Chuo kinatoa fursa ya ajira kwa wanafunzi waliofanya vizuri zaidi, pia kinatoa fursa ya kuwaunganisha Wahitimu na maeneo kwa ajili ya kujitolea (Volunteer) ili kukuza ujuzi wao.
30. Kozi ya ustawi wa Jamii ni nini na unafanya kazi gani baada ya kuhitimu?
- Hospitali za ngazi zote kama Afisa Ustawi wa Jamii,
- Taasisi za serikali kama afisa ustawi wa jamii kata, wilaya na mkoa (Social welfare Officer),
- Kwenye vyombo vya ulinzi na usalama mfano Jeshi la Polisi, kwenye madawati ya jinsia.
- Mahakamani kama probertional officer,
- Taasisi za elimu mfano mashuleni kama mshauri (counselor),
- Mifuko ya hifadhi ya jamii na bima za afya (NSSF, LAPF, NHIF&CHIF,GEPF, LAPF, PPF, PSPF, na WCF),
- Taasisi za kimataifa kama Unicef, World Vision, ICAP International, mashirika ya kusaidia waliopata majanga ya Asili kama Msalaba mwekundu, Kambi za wakimbizi na taasisi nyinginezo nyingi.
- Taasisi zinazohudumia watoto wenye mahitaji maalumu kama vituo vya kulea watoto yatima. Pia Afisa Ustawi wa Jamii anaweza kuhudumu kwenye mashirika ya kutetea haki za binadamu.